• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    WEMA SEPETU: NAWADAI CCM FEDHA ZANGU TOKA 2015


    Malkia wa filamu nchini Wema sepetu amethibitisha kuwa japo amekihama Chama cha Mapinduzi lakini bado alikuwa anadai madeni yake yaliyotokana na kampeni za uchaguzi mkuu alizofanya mwaka 2015 akiwa na wasanii wengine

    Akiongea mbele ya waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wanachama wa Chadema leo hii, Wema amesema walikuwa wanakidai chama hicho yeye na wasanii wenzake wengine lakini wamekuwa wakiambia madeni hayo wakamdai Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.
    “Kuna madeni kweli ambayo wasanii wenzangu wanadai nikiwemo mimi lakini cham kama chama kinajua chenyewe, nikianza kuongelea madeni nitakuwa kama nakumbuka shuka asubuhi,” amesema Wema.
    “Madeni yapo kama hilo ndio swali na wasanii wenzangu wengi wanakidai Chama cha Mapinduzi lakini sasa tumekuwa tunaambiwa tumfuate tumfuate JK. Tumfuate JK tukamdai na maneno mengine mengi ambazo ni fununu tumekuwa tunasikia,” ameongeza.
    Kwa sasa Wema na mama yake ni wanachama wa Chadema.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad