• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    MKUU WA SHULE YA SEKONDARY AJINYONGA SINGIDA


    Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke.
    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake.
    Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo.
    Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe.
    “Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu maana mke wake amekuwa akiishi mbali naye kwa kipindi kirefu sana, amekuwa mpweke kwa muda mrefu mno huenda hicho ndicho kilichosababisha ajitoe roho yake,” amesema Mjumbe huyo wa Bodi.
    Marehemu Makala ni mzaliwa wa kijiji cha Ndago, wilayani Iramba na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake, ameacha mjane na watoto watano.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad