• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    MOURIHNO: ROONEY ANAWEZA KUONDOKA MANCHESTER UNITED


    Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema bado inawezekana Wayne Rooney aihame klabu hiyo mwezi huu.
    Mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 31 alifunga bao lake la 250 United mwezi uliopita na kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo.
    Hata hivyo, kumekuwa na uvumi kwamba huenda akahamia China.
    Soko la kuhama kwa wachezaji Ligi Kuu ya China litafungwa wiki ijayo.
    Mourinho aliulizwa iwapo nahodha huyo wa United atakuwa Old Trafford kufikia wakati huo.
    "Itabidi mumwulize mwenyewe," Mourinho alisema.
    "Bila shaka siwezi kuwahakikishia (kwamba atakuwa hapa). Siwezi kuwahakikishia kwamba nitakuwa hapa wiki ijayo, nitawezaje kuwahakikishia kwamba mchezaji atakuwa hapa msimu ujao?"
    Mkataba wa Rooney United ni wa hadi 2019 na majuzi alikuwa amedokeza kwamba kuna uwezekano huenda asimalize muda wote huo United.
    Amekuwa hapewi nafasi ya kuwa katika kikosi cha kuanza mechi msimu huu na amefunga mabao matano pekee.
    Hata hivyo, Mourinho alisema Oktoba kwamba Rooney hakuwa anenda "popote" na alisisitiza Jumanne kwamba hataki mchezaji huyo aihame Manchester United.
    "Siwezi kumsukuma - au kujaribu kumsukuma - nyota wa klabu hii ahame," aliongeza Mourinho.
    "Hivyo, itabidi mumwulize iwapo anaona kama atakuwa katika klabu hii kipindi kilichosalia cha uchezaji wake au iwapo anadhani atahama.
    "Si swali langu hilo kwa sababu ninafurahia kuwa naye. Sitaki aondoke."

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad