ALIKIBA AJIBU KAULI YA DIAMOND PLATNUMZ
Jitihada za kuitafuta amani kati ya Diamond na Alikiba zinaweza zisizae matunda leo wala kesho. Kama unakumbuka, kwenye interview ya Clouds TV, Diamond alisema kuwa hajawahi kuwa na tatizo na Alikiba na kwamba atapenda kupata pia muziki wake kwenye website ya Wasafi.com. Usiku wa Jumanne Kiba alijibu kauli hiyo kimafumbo na kuashiria kupingana na kile alichokisema hasimu wake.
Aliandika kwenye Instagram, “Umeshatibua Mavumbiee Unatafuta Pa kuhemeaaa 🎶
#KingKiba.
#KingKiba.
Baadaye aliongeza nyingine: Waambie Wasituzoee kabisa MAZOEA kuzoeana 🎶🎶 @billnass #alikibaworldtour2k17
#KingKiba.
#KingKiba.
Kama haitoshi, aliongeza post nyingine ya video ikimuonesha mtoto akitoa ushauri kuhusu kutorudi nyuma ama kujihusisha na ushindani. Post za Alikiba zimesababisha mjadala mkubwa huku wengi wakimshutumu kwa kuendekeza ugomvi ambao mwenzake ameonesha kutotaka uendelee.


No comments