• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    CHRISTIAN BELLA: NACOPY KILA KITU KWA CHRIS BROWN


    Mkali wa muziki wa Dance hapa Tanzania Christian Bella, ambae kwa sasa anafanya vizuri na chupa la ngoma yake “Ollah” akiwa amemshirikisha rapper kutoka Kenya Khaligraph Jones, huku chupa la ngoma hiyo likiwa limeongozwa na Hanscana.
    Christian Bella amefunguka na kusema kuwa mara nyingi hata ‘idea’ ya muziki wake zinatoka kwa msanii Chris Brown kutoka Marekani na kusema ni kati ya wasanii ambao anasikiliza sana kazi zao.
    Christian Bella amedai kuwa anapenda kusikiliza sana kazi za Chris Brown kwanza ni kutokana na ukweli kwamba anampenda msanii huyo lakini pia kingine ni kutokana na majina yao kufanana.
    “Mimi kusema kweli sina ‘Role model’ bali mimi napenda muziki mzuri lakini kwa kizazi chetu ukiangalia kwa nje nampenda sana Chris Brown na nasikiliza sana kazi zake, kwa sababu kwanza tunaendana majina ( CB )  Christian Bella, Chris Brown, yaani na mimi ni Breezy vile vile.
    Aliongeza, “Yaani jamaa ana flow flani ambazo mimi mwenyewe nikimsikiliza nasikia raha lakini hata njia zake pia na feeling zake naposikiliza huwa zinanipa idea, zinanisaidia idea za kuimba lakini huwezi kuelewa kwamba kuna flow flani kwenye kazi zangu kupitia kumsikiliza Chris Brown ndiyo niliweza kuzipata” alisema Christian Bella ndani ya EATV.
    Mbali na hapo Christian Bella amesema kwa wasanii wa bendi, msanii anayemkubali na kusikiliza sana kazi zake ni Koffi Olomide, kwani anadai msanii huyo amefanya mambo makubwa sana kwenye muziki wa dansi nchini DRC.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad