• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    MWANAMKE ACHOMWA MOTO HADI KUFA


    MWANAMKE mkazi wa Managua, amekufa baada ya kufungwa kamba na kurushwa kwenye moto na watu wanaodhaniwa wafuasi wa dhehebu la dini kwa lengo la kuteketeza mapepo.
    Watu wa familia yake wameviambia vyombo vya habari kuwa, Vilma Trujillo (25) alishambuliwa na watu wanne wakiongozwa na mtu aliyetajwa kuwa ni mhubiri.
    Mhubiri huyo, Juan Rocha amekusha tuhuma za kumuua mwanamke huyo kwa kumchoma moto.
    Amedai kuwa, Trujillo amekufa kwa kuwa pepo wabaya walimchukua mwanamke huyo na kumrusha motoni.
    Mwili wa mwanamke huyo ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa ya moto.
    Maofisa wa polisi walimkamata Rocha na watu wengine wanaohusishwa na tukio hilo la kumchoma kwa moto Trujilo.
    Mume wa mwanamke huyo, Reynaldo Perlata Rodriguez amesema mkewe alichukuliwa na kupelekwa kanisani wiki iliyopita wakati wafuasi wa kanisa hilo walipodai ana mapepo baada ya kujaribu kuwashambulia watu kwa panga.
    “Hatuwezi kuwasamehe kwa kile walichotufanyia, alinukuliwa akisema. Walimuua mke wangu mama wa watoto wangu wawili. Nitawaambia nini watoto wangu?” amesema.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad