• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    NAY AZUNGUMZIA NDOTO YA KUWA MCHUNGAJI


    MKALI wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa, kwa sasa anawaza jinsi ya kujenga kanisa ili watu wamwabudu Mungu lakini hana ndoto za uchungaji kwa sababu haijui Biblia vizuri.
    Akistorisha na Risasi Vibes, Nay alisema kuwa, baada ya kutangaza kujenga kanisa ambalo watu hawatatoa sadaka litakuwa kwa ajili ya kumwabudu Mungu, watumishi wengi wa Mungu walishtushwa na kauli yake hivyo anawatoa wasiwasi kwamba hana mpango wa kuwa mchungaji.
    Alisema kuwa, yeye atajenga kanisa maeneo ya MbeziMwisho, Dar na watakuwepo wachungaji kwa ajili ya kuwafundisha watu Neno la Mungu na siyo yeye kama yeye.
    “Sina ndoto za kuwa mchungaji maana sijui hata Neno la Mungu vizuri, nimeguswa kujenga kanisa tu ili watu wamwabudu Mungu kwa kuwa amenijalia kipato hivyo nafanya kama kutoa shukurani kwake. Kanisa hilo halitakuwa kwa ajili ya sadaka bali kumwabudu Mungu,” alisema Nay.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad