• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    VIDEO: BARCELONA YAIUA PSG 6-1 WASHANGAZA ULIMWENGU


    Usiku wa kuamkia leo club ya Fc Barcelona imeweka historia ya aina yake pamoja na kushangaza ulimwengu kwa kuweza kuwafunga wageni wao kutoka Ufaransa  PSG jumla ya magoli 6-1

    Mechi ilikuwa na mvuto wa aina yake kutokana na barcelona kushambulia kwa kasi kutoka mwanzo wa mchezo mpaka mwisho

    Wafungaji wa magoli hayo ni:

    Luis Suarez aliiandika BARCELONA goli la kwanza dakika ya 3' Ikifuatiwa na Kurzawa aliyejifunga dakika ya 40' na kufanya kumalizika kwa kipindi cha kwanza BARCELONA ikiongoza jumla ya magoli 2-0

    Kipindi cha pili Barcelona walijipatia bao la tatu dakika 50' kupitia kwa LIONEL MESSI aliyefunga kwa mkwaju wa penati na hatimaye PSG wakapata goli la kufutia machozi kupitia kwa EDSON CAVAN dakika ya 62'

    NEYMA JR hakuwa nyuma baada ya kupiga magoli mawili dakika ya 88' na 91' kwa njia ya free kick na penati na SERGI ROBERT akahitimisha na kuwapelekea msiba WAFARANSA PSG kwa kupiga goli la mwisho dakika za nyongeza kutokana na mpira wa adhabu uliopigwa na NEYMAR JR

    Ushindi huo unaipeleka BARCELONA hatua inayofuata kwa jumla ya magoli 6-5 baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa nchini ufaransa kufungwa na wenyeji PSG 4-0

    STAR255 TV inakutelea video ya magoli yote kwa kutazama hapa chini




    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad