SHILAWADU WAPEWA LIKIZO KISA RC MAKONDA
Watangazaji Soudy Brown na Qwhisar Thompson wa kipindi cha The Weekend Chart Show cha Clouds Tv wape likizo fupi kufuatia sakata la Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za CLOUDS MEDIA kwa mitutu ya bunduki usiku wikendi iliyopita.Akizungumza kupitia Clouds 360 mkurugenzi wa vipindi wa vipindi Ruge Mutahaba ameonesha kutoridhishwa na tukio lile na kusema kuwa kosa kubwa linalojitokeza ni kiongozi kutaka juu zaidi kwa mgongo wa madaraka aliyoanayo
Kutokana na joto la sakata hilo kuwa juu watangazaji hao wawili wamepewa likizo kutokana na kuhofia kukosa amani na uhuru wa kuendelea na kipindi chao hicho laimaarufu kama SHILAWADU.
Hata hivyo Mkurugenzi ameongeza kwa kusema kuwa Paul Makonda ameikosea heshima taasisi hiyo ya habari.

No comments