• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    VANESSA MDEE KUACHIA NGOMA WIKI HII


    Kwa misukosuko aliyoipitia Vanessa Mdee hivi karibuni sio rahisi kufikiria kuwa msanii huyo ana nguvu ya kuachia kazi mpya kwa sasa, lakini kwa mujibu wa tweets zake za jana ni wazi kuwa changamoto alizokumbana nazo zimempa morali kubwa zaidi.
    Akiwa miongoni mwa wasanii waliotajwa kwenye list ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, Vanessa Mdee siku ya Machi 13 2017 aliachiliwa kwa dhamana na siku mbili badaae alirudi mtandaoni kusema na mashabiki wake.  
    Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Vee Money aliwashukuru mashabiki kwa kuonyesha upendo mkubwa juu yake na kusema tutegemee kazi mpya kutoka kwake wiki hii.

    “Kama ulikuwa unawaza juu ya maendeleo yangu. Naendelea vizuri sana. Isitoshe ngoma mpya inatoka WIKI HII” – Alisema Vanessa kupitia Twitter page yake. 
    Mbali na hilo la kutegemea kazi mpya kutoka kwa ‘Cash Madame’, Vanessa Mdee ataungana na msataa waNigeria kama DavidoBurna BoySeyi Shay na Reekado Banks wa Mavin Reords kutumbwiza kwenye tamasha kubwa la muziki nchini humo ‘Gidi Fest’ linalotegemea kufanyika mwezi wa nne kwenye msimu wa sikukuu za pasaka.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad