• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    RASMI FROLA MBASHA ACHUMBIWA ABADILI NA JINA


    Baada ya wanandoa ambao ni wanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili, kuingia katika mzozo miaka minne iliyopita, mmoja wao Flora Mbasha amechumbiwa na anatarajiwa kufunga ndoa ya pili hivi karibuni mkoani Mwanza.
    Sakata hilo linaweza kuibua mjadala miongoni mwa waumini wa dini ya Kikristo ambayo pamoja na kuruhusu ndoa kuvunjika, ni nadra sana kwa makanisa kuidhinisha suala hilo.
    Habari za kuaminika  zinasema vikao vya maandalizi ya harusi hiyo vimeshaanza baada ya Flora kufanikiwa kupata talaka aliyoidai Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini hapa.
    Flora, ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa muhubiri maarufu nchini, Askofu, Moses Kulola (sasa marehemu), tayari amevishwa pete ya uchumba na amebadili jina la kisanii akitaka mashabiki wake wamtambue kama “Madame Flora” badala ya jina aliloibukia la Flora Mbasha.
    Asili ya neno “madame” analotumia Flora ni Ufaransa na linamaanisha mwanamke aliyeolewa.
    “Kwa sasa siwezi kukwambia chochote kuhusu hilo. Sijui, labda ifikapo Machi naweza kuzungumza,” amesema Flora, ambaye alitamba na kibao cha “Jipe Moyo”.

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad