SONY MUSIC KUMUINUA WIZKID KIMATAIFA MWAKA HUU
Ni nadra sana kukuta msanii wa Afrika anafikiriwa kuwa kipaumbele kwa lebo yoyote kubwa ya kimataifa hasa kama Sony Music, lakini kwa nyuzi kali za Bad Man Wizzy ni wazi kuwa wasanii kutoka Afrika wamekuwa wagumu kuwapotezea.
Mkali wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahim ‘Wizkid’, adaiwa kuwa ndani ya mwaka huu project zake nyingi zitapewa backup kubwa sana na lebo ya kimataifa Sony Music, na kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, Sony Music imetangaza kuwa kwa mwaka huu Starboy Wizzy ni kipaumbele chao cha kwanza kuhakikisha kuwa staa huyo anafikia malengo yake ya kuwa a Super International star.
Sony Music kupitia wakurugenzi wake wa RCA Records wamethibitisha tetesi zinazosambaa juu ya maamuzi hayo kupitia press statement inayosema.. “New RCA priorities in 2017 include 18-year-old Texan Khalid, All My Friends singer Tinashe, Nigerian One Dance collaborator Wizkid, hip-hop artist Goldlink and band Muna.”

No comments