• MUHIMU

    NDUGU MSOMAJI WETU ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU SASA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO/MUZIKI WAKO NASI KWA BEI NAFUU SANA AMBAYO ITAKUFANYA UWIFIKIWE NA WATEJA WENGI NCHINI.PIA TUNATOA HUDUMA ZA BLOG DESIGN NA ANDROID APLLICATION TUPIGIE 0655569428 AU FOLLOW INSTAGRAM @star255com FACEBOOK:sta255 TWITTER: star255_ KARIBUNI SANA.>>

    YOUNG DEE RASMI ATASIMAMIWA NA MR T TOUCHEZ ( TOUCHEZ SOUNDS)

    Mtayarishaji wa muziki wa bongo fleva  Mr T Touchez anayefanya vizuri kwa kutengeneza hits kibao amesema msanii Young Dee amejiunga na label yake ya Touchez Sound na tayari wana project zaidi ya sita.
    Akiongea na eNewz ya EATV, Mr T Touchez amesema Young Dee yupo kwenye lebo yake ya Touchez Sound na kwa sasa ana meneja wake ambaye anamsimamia na pia tayari wameshatengeneza nyimbo zake zaidi ya sita lakini pia muda wowote kuanzia sasa ngoma mpya ya Young Dee itakuwa hewani.
    Hata hivyo Mr.T Touchez alimalizia kwa kusema “Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee na ataendelea kuwepo chini ya Touchez Sound na mimi ndiye nitakayesimamia na kutengeneza biti za nyimbo zake zote na nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi namuona ni msanii mwenye biashara

    No comments

    Post Top Ad

    Post Bottom Ad